D
Wananchi TV DPROMO Vigezo na Masharti ya Huduma

Vigezo na Masharti (Terms of Service)

Tarehe ya Mwisho Kuboreshwa: 27 Agosti 2026

1. Kukubaliana na Masharti

Kwa kutembelea tovuti ya dpromo.wananchi.tv.tz na kutuma maombi ya huduma zetu za matangazo ya kidijitali, unakubaliana na vigezo na masharti haya.

2. Ufafanuzi wa Huduma

Wananchi TV DPROMO inatoa huduma ya kusimamia na kuendesha kampeni za matangazo ya biashara kwenye majukwaa ya Meta (Facebook & Instagram) kwa lengo la kuleta wateja kwenye WhatsApp ya mteja (Sales/Conversations).

3. Wajibu wa Mteja na Bidhaa Halali

  • Mteja anawajibika kuhakikisha bidhaa au huduma anayotangaza ni halali kulingana na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sera za matangazo za Meta (Meta Advertising Standards).
  • Hairuhusiwi kutangaza bidhaa zilizopigwa marufuku (kama dawa za kulevya, silaha, au miradi ya udanganyifu).

4. Malipo na Bajeti ya Tangazo

DPROMO haikatwi fedha moja kwa moja kwenye kadi ya benki ya mteja. Malipo ya bajeti ya tangazo yanafanywa na kuthibitishwa moja kwa moja kupitia njia rasmi za malipo za Wananchi TV.

5. Haki Miliki na Uhuru wa Ukurasa

Mteja anabaki kuwa mmiliki halali wa ukurasa wake wa Facebook na akaunti ya Instagram. DPROMO inapokea ruhusa ya uendeshaji wa matangazo pekee bila kubadilisha umiliki wa ukurasa.

← Rudi kwenye Ukurasa Mkuu